Baada ya
kushuhudia michezo ya hapo jana katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, michezo mingine
ya hatua ya 16 bora itapigwa tena hii leo ambapo Arsenal watakuwa nyumbani
kucheza na Monaco katika pambano litakalopigwa katika uwanja wa Emirates.
Mchezo huo
utakuwa wa hisia kubwa sana kwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwani amekwisha wahi
kuifundisha timu ya Monaco kuanzia mwaka 1987 na 1994 huku akishinda vikombe
vya Ligi kuu ya soka nchini Ufarana na kombe la Ligi la Ufaransa maarufu kama
Coupe De France.
Arsenal
wataingia uwanjani pasipokua na nyota wake Aaron Ramsey ambaye ni majeruhi, Abou
Diaby, Jack Wilshere na Alex Chamberlain wakati Monaco wao watawakosa Toulalan na Traore.
Mchezo
mwingine utakuwa kati ya Bayer 04 Levekusen dhidi ya Atletico Madrid.
Arsene Wenger akijiandaa wakati akiwa meneja wa club Monaco, hii leo wanakutana.
Wenger akiwa na furaha ya kukutana na timu yake ya zamani katika hatua ya 16 ya Uefa champions ligi.
Wenger wakati anaihudumia Monaco enzi hizo
0 comments:
Post a Comment