Makamu wa Rais wa zamani wa
shirikisho la soka nchini TFF na mjumbe wa kamati ya rufaa ya shirikisho la
soka barani Afrika CAF Athumani Nyamlani ndiye atakayefungua mashindano ya DR. MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP 2014.
Mashindano hayo yanayoshirikisha
timu 32 yanaanza kwa mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya Friends Rangers dhidi
ya Kiluvya United katika uwanja wa mwalim nyerere makulumla magomeni.
Mchezo huo utaambatana na
matukio mbalimbali ikiwemo burudani ya muziki wa kizazi kipya ambapo
Makomandoo, Msaga Sumu na Mataluma wataburudisha kuanzia saa saba mchana.
Mashindano hayo yanaletwa
kwa udhamini wa Dr Mwaka ambaye ni
mtaalam wa masuala ya afya ya uzazi kutoka kituo cha Foreplan clinic kilichopo
Ilala Bungoni Dar es salaam, Clouds fm
na Clouds tv.
Tunasema
heshima ya soka la mtaani imerudi…..
0 comments:
Post a Comment