Angel di
Maria aliyekuwa patna wa mchezaji christian ronaldo katika klabu ya Real Madrid amekabidhiwa jezi No 7 Manchester United iliyokua ikivaliwa na ronaldo wakati akiichezea klabu hiyo.
Di
Maria, ameingia mkataba wa miaka 5 na klabu hiyo ambapo atakua akilipwa paund laki mbili (200,000) kwa wiki, amepewa jezi hiyo ambayo imewahi kuvaliwa na wachezaji wenye majina makubwa man u akiwemo Ronaldo, Eric Cantona na David Beckham.
Di Maria ni mchezaji wa kimataifa wa Argentina alitambulishwa rasmi siku ya alhamisi.
Angel Di Maria amesema Cristiano Ronaldo alimwambia avae jezi No 7 Manchester United
Di Maria akitembezwa katika uwanja wa old Traford na meneja wake Vaan Gaal
0 comments:
Post a Comment