Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekitaka chama chake cha ZANU-PF
kimtafute mtu atakayemrithi.
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 89 na
ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980, amewataka viongozi wa chama
cha ZANU-PF waanze kufikiri mtu atakayemrthi yeye.
Rais Mugabe ambaye hakusema wazi na bayana kama hana mpango wa
kuendelea kuwa madarakani amesema hayo kabla ya kufanyika mkutano mkuu
wa kila mwaka wa chama tawala cha ZANU-PF.
Matamshi hayo ya Rais Mugabe yametathminiwa kwamba, ni tangazo lisilo
rasmi la kiongozi huyo mkongwe barani Afrika la kutaka kung'atuka
madarakani.
Hivi karibuni Rais Mugabe alisema katika moja ya vikao vya
chama kwamba, kiongozi ajaye wa ZANU-PF anapaswa kuchaguliwa na mkutano
mkuu wa chama hicho.
Kwa mujibu wa redio tehran
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment