Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania, Profesa
Ibrahim Lipumba amesema kuwa, mchakato wa Katiba Mpya nchini humo una
vikwazo vingi na kwamba Katiba haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama Rais
Kikwete alivyoahidi, hivyo kuna haja ya kuunda Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Bara. Hii ni mara ya pili kwa Lipumba kutoa kauli hiyo.
Mei mwaka huu, mwenyekiti huyo wa CUF taifa alitoa tamko kama hilo
alipoonyesha wasiwasi wake kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya na akasema
kwamba, ni hila za CCM za kutaka kumwongezea muda Rais Kikwete.
Profesa
Lipumba ametaja baadhi ya vikwazo ambavyo vinaweza kukwamisha kupatikana
kwa Katiba mpya kuwa ni Daftari la Kudumu la Wapigakura kama
halijaboreshwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho vya utaifa
ambavyo vitatumika kupigia kura hiyo.
Wakati Profesa Lipumba akisema hayo, tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(Nec), imeeleza kuwa haina mpango kwa sasa wa kuboresha Daftari la
Kudumu Wapigakura kwa ajili ya kura za maoni kwa sababu muda uliobaki ni
mfupi.
Kwa mujibu wa radiotehran
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment