MALINZI KUFUNGUA MICHUANO YA UHAI 2013
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafungua
rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.
Uzinduzi
wa mashindano hayo utafanyika kesho (Novemba 17 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa 2 kamili asubuhi.
Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal Union.
Mechi
nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Uwanja
wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi-
Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Uwanja wa Karume).
Kundi
C kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa
saa 2 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex, na kwenye uwanja huo
huo saa 10 jioni ni Rhino Rangers dhidi ya Tanzania Prisons.
RAMBIRAMBI MSIBA WA NYOTA COPA COCA-COLA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa Sayari, Fatuma Bahau ‘Crouch’ kilichotokea jana (Novemba 15
mwaka huu) kwenye Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa katika mpira wa miguu kwani Fatuma ndiyo kwanza alikuwa
anachipukia katika mpira wa miguu wa wanawake ambapo alikuwa mfungaji
bora wa michuano ya U15 Copa Coca-Cola ya mwaka huu akichezea timu ya
Ilala, hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.
Kwa
mujibu wa mlezi wa mchezaji huyo, Stephania Kabumba, marehemu
anasafirishwa kesho kwenda kwao Mwanza kwa ajili ya maziko ambapo kifo
chake kimesababishwa na ugonjwa wa malaria.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bahau, klabu ya Sayari, Chama cha
Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Fatuma mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment