Main Menu

Wednesday, November 20, 2013

KIARANJA KUWAANGAMIZA WAKENYA NA MOURINHO NA AMANI YA TIMU YA TAIFA YA HISPANIA

Kiaranja kuwaangamiza wakenya na Mourinho na amani ya timu ya taifa ya Hispania,.......::.. Ngugi wathiong'o kwenye ubora wake aliwahi kuandika kitabu chake akakiita a grain of wheat kinazungumzia kwa kifupi harakati za maisha ya wakenya katika kupata uhuru kamili.

Kuna visa vingi lakini mimi binafsi siku ya leo ntamzungumzia karanja na kwenye mipango ya kutoitakia mema nchi ya kenya ingawa alikuwa ni mkenya ambaye hakutaka kufuata sera za wenzake yeye aliona wakoloni ni kila kitu na ndio maana aliwasaliti wakenya.

Ukienda roma unatakiwa uuvae utaratibu wa roma jose mourinho alipo fika nchini hispania aliwakuta wahispaniola wakiwa na furaha kubwa kutokana na kiu yao ya miaka minne ya kufanya vizuri kwenye soka baada ya kusubiri kwa miaka kenda.

Mourinho aliingiza sera zake kwenye klabu ya real madrid special one alifanikiwa kupata nafasi ya kuiongoza madrid kwenye michezo 11 ya elclasico hii ilikuwa kabla ya michuano ya euro 2012 katika michezo hiyo kadi 82 za manjano zilipatikana kwenye elclasiko hizo, 9 nyekundu pia mourinho na msaidizi wake karanka waliadhibiwa kutokana na vurugu uwanjani.
 
Mourinho alihusika na matukio ya uhalifu uwanjani kwani alitaka kusababisha xavi na Casilas nusura wazichape kutokakana na shinikizo kutoka kwa mourinho, unajua kwanini mtu huyu maalumu alihatatarisha maisha ya wahispaniola waliokuwa wanaiombea la roja ikatetee la mataifa ya ulaya mwaka 2012.

Kitu pekee kilichomfanya mourinho aharibu mipango kazi iliyoanzishwa na vicente del bosque na mtangulizi wake luis aragones ni kutaka kuuvunja umoja wa kitaifa uliokuwa awali unatengenezwa na wachezaji wa laroja ambao kwa kiasi kikubwa ni nyota wa real madrid na barcelona.

Mourinho kama alivyo karanja kwenye a grain of wheat alitanguliza maslahi yake mbele kuliko ya hispania tatizo ni mchezo wake wa kwanza dhidi ya barca alipigwa 5 hivyo akaamua kupandikiza chuki miongoni mwa wanafamilia wa la roja kwa kuwahamasisha wachezaji wa real wawachukie wa barca, na kusahau kua msingi mkubwa wa timu ya taifa ni vilabu.

Del bosque alitumia muda mwingi kuwaunganisha nyota wa hispania ambao miaka miwili nyuma nazungumzia 2010 walivyoweza kusherehekea ubingwa wa dunia kwenye ardhi ya afrika ilishangaza nyota hao kuchukiana hadharani kwenye elclasico na nje.

Del bosgue alipata shida lakini alifanikiwa kupata taji la euro 2012 na uliopandikizwa na mourinho ulihamia kwenye timu ya real madrid ambapo aliigawa timu kwa wachezaji wa kireno pia kwa wahispania cr7 akawa haivi na Casilas yote ilikuwa mourinho akitaka atajwe sana yeye kuliko kundi la wachezaji au mchezaji mmoja mmoja timu ikakosa mwelekeo na baadae wale madrista ambao pia wanamioyo ya kihispania walipomtoa mbio mourinho kama karanja alipogundulika kuwa yeye ndiye chanzo cha kihika kufungwa jela.

Pia yeye ndiye aliyekuwa anadunisha harakati za wakenya kwenye kujipatia uhuru, bila busara za Del bosque na madirista Spain ingelisikia bombani kombe la dunia lijalo.

Amani imerejea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya timu ya taifa Hispania, baada ya kuondoka kwa Karanja a.k.a Mourinho hata Elclasico ya kwanza msimu huu iliyofanyika tarehe 26 mwezi wa 10 mwaka huu kwenye dimba la Nou Camp haukuwa na vitendo vya kihuni vilivyozoeleka kwa miaka mitatu iliyopita.

 
pia timu ya spain a.k.a La Roja amani imerejea tena kwenye kikosi hicho hata xavi hernandez anajiuliza kwanini alitaka kupigana na kasilas, kwanini kasilas haanzi kwenye kikosi cha Real? pia Sergio Bosquet kwa mara ya kwanza  toka alivyo hivyo hadharani nchini Afrika kusini amemsifia Kasilas kuwa ni mmoja ya watu muhimu kwenye kikosi cha La roja. 

Enzi za Mourinho nchini Hispania hakuna mchezaji wa Barca aliyekuwa na uwezo wa kutoa tabasam hata feki kwa mchezaji wa Real Madrid pindi wanapokutana kwenye kikosi cha timu ya taifa.

Muharibifu kaondoka na  spain itasonga kama awali.

Makala hii imeandaliwa na issa maenda wa ebony fm

0 comments:

Post a Comment