Main Menu

Thursday, November 21, 2013

MAHAKAMA YA RUFAA YATUPILIA MBALI RUFAA YA BABU SEYA NA PAPII KOCHA


Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali rufaa ya mwanamuziki wa dansi Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Papii Kocha ya kutaka adhabu ya kifungo cha maisha iliyotolewa na mahakama hiyo February 2010 ipitiwe upya.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka mahakamani hapo, mahakama imesema kuwa hakukua na sababu za msingi ambazo zingepelekea mahakama hiyo kupitia upya hukumu hiyo kwa kuwa utetezi walioutoa Nguza na mwanae unafanana na utetezi wa awali waliotoa kwenye shauri hilo.

Hii inamaanisha kuwa Mwanamuziki huyo mkongwe na mwanae wataendelea na adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Nguza Vicking na mwanae walihukumiwa kifungo cha maisha jela February 2010 baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji na ulawiti.

0 comments:

Post a Comment