Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefutwa kazi na
kufungwa jela kwa kitendo cha uporaji waliofanya wakati wa shambulizi la
kigaidi dhidi ya jengo la Westgate mwezi jana.
Hii ni kwa mujibu wa
mkuu wa jeshi Julius Karangi.
Wanamgambo wa Somalia, al-Shabaab walikiri kufanya shambulizi hilo ambapo waliteka nyara wakenya kadhaa waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Watu 67 walifariki na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Wakati huohuo, mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa uhalifu katika idara ya polisi,Ndegwa Muhoro alisema kuwa mmoja wa magaidi waliokuwa ndani ya jengo hilo walipiga simu nchini Norway wakati walipovamia jengo hilo.
Mmoja wa washukiwa wa shambulizi hilo ametajwa kuwa Hassan Abdi Dhuhulow mzaliwa wa Somalia ingawa raia wa Norway.
Jeshi limesema kuwa magaidi wote wanne waliofanya shambulizi hilo waliuawa.
Lakini katika ripoti za awali, iliarifiwa kuwa washambuliaji walikuwa kati ya kumi na kumi na watano.
Bwana Muhoro alisema kuwa watu wengine watano wamezuiliwa kwa uchunguzi zaidi na kuwa watafikishwa mahakamani hivi karibuni.
na bbcswahili.com
0 comments:
Post a Comment