Baada ya fans wengi kuanza “kumponda” mwanadada Irene Uwoya kuwa
gari aina ya Range Rover aliyoinunua “amehongwa na washika dau”,
mwanadada huyo ameibuka na kusema kuwa mali anazomiliki amezinunua kwa
pesa zake anazopata kwenye uigizaji pamoja na zile zinazotokana na
biashara zake nyingine.
“Kwa nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa,
yaani sisi tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na
si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya.
Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri
kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza
kupata mafanikio makubwa.
“Tunaigiza sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii
siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta
unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema
Irene amesema kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na
maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume
‘wanaomweka mjini’.
NA bongomovie.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment