Main Menu

Sunday, October 27, 2013

BABA MZAZI WA WEMA SEPETU,BALOZI ISAAC SEPETU AFARIKI DUNIA


Taarifa iliyoifikia kiujamaazaidi.blogspot asubuhi hii,inaeleza kuwa Balozi Issac Abraham  Sepetu ambaye pia ni Baba mzazi wa Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu.Amefariki Dunia asubuhi ya leo kwenye Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinasema kuwa,Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.

Hadi Mauti yanamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Kiujamaazaidi.blogspot inaungana na Waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu,Aiweke Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.

Amen.


0 comments:

Post a Comment