Main Menu

Sunday, October 27, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 USIKU WA JANA NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR.



 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Amin na Linah wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta kwa pamoja .
 Baadhi ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Amin na Barnaba wakiimba kwa pamoja mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake (hawapo pichani) .
 Pichani juu na chini ni mwanamuziki Alain Laughton kutoka nchini Jamaica,akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la dar (hawapo pichani).  
 Mwanamuziki Alain Laughton kutoka nchini Jamaica,akiimba kwa hisia huku akipiga kinanda jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la dar (hawapo pichani).
 Mmoja  wasanii wa kike wa bongofleva aitwaye Recho, ambaye mara nyingi amekuwa akifananishwa na msanii aliyewahi kuwika kwenye anga ya muziki huo Ray C,pichani kati akilishambulia vilivyo jukwaa la fiesta na madansa wake.
 Mwanamuziki wa Bongofleva,Recho akiimba na mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C  kwenye jukwaa la fiesta 2013,ambapo muonekano wake uliwashtua wengi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii H Baba akitumbuiza mbele ya mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta  kwenye viwanja vya Leaders Club jijini  Dar.
 Sehemu ya mashabiki wakishangweka.


Hata hivyo tamasha hilo halikwenda kama lilivyopangwa kutokana na matatizo ya kiufundi na kusababisha baadhi ya wasanii kushindwa kupaform.

Kutokana na matatizo hayo waandaaji wa tamasha hilo prime time entertainment imewaomba radhi wananchi wote waliojitokeza na kwa kuwaheshimu tamasha hilo linafanyika tena leo mchana ambapo wasanii kibao watapiga show akiwepo Diamond, Davido, Ney wa mitego na wengine wengi kwa kiingilio cha bure yaani miguu yako tu kufika leaders club.

PICHA NA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

0 comments:

Post a Comment