Warembo wakiendelea na mazoezi ya mwisho mwisho kuelekea misii redds miss iringa 2013 itakayofanyika katika ukumbi wa Highlands usiku wa ijumaa ya tarehe 14 june.
Walimbwende katika pozi mbalimbali wakati wa mazoezi club la parte inayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni mkoani Iringa.
Maandalizi kwa ajili ya redds miss iringa mwaka 2013 yanaendelea vizuri na yakiwa katika hatua za mwisho kabisa wakati warembo tisa wakiendelea na mazoezi yao chini ya wakufunzi miss iringa namba moja mwaka 2012 na mwaka 2011.
Akizungumza na mtandao huu mratibu wa shindano hilo Doss Magambo amesema kila kitu kinakwenda vizuri na warembo wote wamewasili katika mazoezi.
Katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika ijumaa ya tarehe 14 june, Magambo amesema tayari tiketi za awali kwa ajili ya shindano hilo zimeanza kuuzwa kwa kiasi cha shilingi 12,000/= tu kwa viti vya kawaida na vip shilingi 30,000.
Magambo ameongeza kuwa tiketi hizo kwa siku ya tukio zitauzwa shilingi 15,000 hivyo katoa wito kwa wakazi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake kuchangamkia nafasi hiyo.
Amesema kuwa tiketi za awali zimeanza kupatikana katika ofisi za Ebony fm Iringa, Nems Collection, na Maama Beauty Saloon Tumaini.
Shindano hilo la Redds Miss Iringa mwaka huu limeandaliwa na Ebony Entertainment na kudhaminiwa na REDDS ORIGINAL, PEPSI DARE FOR MORE, GLORY LORGE, MKWAWA MAGIC SITE, BWAWANI CAMP SITE, MAAMA BEAUTY SOLOON TUMAINI, NEMS COLLECTION, SISTER D BEAUTY SALOON UHINDINI NA EBONY FM RADIO.
0 comments:
Post a Comment