Hatimaye Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Kamanda Wilfred
Muganyizi Lwakatare 'Lwaks' leo atapata dhamana na kurudi uraiani, baada
ya Mahakama ya Kisutu kuamua kuwa dhamana yake iko wazi na sasa
masharti tu ndiyo yanakamilishwa.
Lwakatare anapata dhamana, huku jaribio la watawala kwa kutumia vyombo
vya dola, kutaka kukichafua kwa kukipaka matope ya ugaidi na mauaji
CHADEMA likiwa limeshindwa vibaya.
It's has been a battle, very seriuos battle, legally and politically, of
almost three months. Bungeni, kwenye majukwaa ya siasa na mahakamani.
Fighting for justice, hopes and dignity of being.
And the battle still goes on. Aluta continua.
Mapambano yataendelea kwa sababu sasa tunaanza kuamini kuwa akina
Hitler, Botha na wengine wa namna hiyo bado wanaishi kwa namna nyingine,
kupitia baadhi ya watu waliokabidhiwa madaraka ya kuongoza lakini
wameamua kutawala.
Usikubali kufumbia macho uonevu wowote, mahali popote, kwa mtu yeyote.
Ukikaa kimya leo, akina Hitler wetu hawa wa zamu zetu, watakapokufikia
wakati wa 'zamu' yako hakutakuwa na mtu wa kukusemea.
Ni muhimu makamanda wasimame kwenye haki, utu, upendo, kweli na
matumaini kwa ajili ya Watanzania hawa wanyonge. Mengine yote yatafuata.
Asanteni kwa kuonesha nguvu ya umma (people's power) kwa kufuatilia
suala hili tangu siku ya kwanza na hadi litakapofika mwisho kwa namna
nyingine linavyoendelea sasa mahakamani.
Tunaanza Mungu, tunaendelea Mungu, tutamaliza na Mungu...
Makene
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
WAOOOH
Post a Comment