Msafara
wa timu ya Taifa ya Ivory Coast (The Elephants) wa watu 80 wakiwemo
wachezaji 27 unatarajiwa kuwasili nchini kesho (Juni 13 mwaka huu) kwa
ndege maalum kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
Mechi
hiyo itachezwa Jumapili (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 9 kamili alasiri, na itachezeshwa na Charef Mehdi
Abdi kutoka Algeria.
Kikosi
hicho kitawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
saa 2.50 usiku na kitafikia hoteli ya Bahari Beach iliyoko nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam. Timu hiyo inatarajia kuondoka saa chache baada
ya mechi hiyo.
Wachezaji
walioko katika kikosi hicho ni Abdoul Razak, Akpa Akpro Jean-Daniel
Dave Lewis, Angoua Brou Benjamin, Arouna Kone, Aurier Serge Alain
Stephane, Bamba Souleman, Barry Boubacar, Boka Etienne Arthur, Bolly
Mathis Gazoa Kippersund, Bony Wilfried Guemiand, Cisse Abdoul Karim,
Diarrassou Ousmane Viera na Dja Djedje Brice Florentin.
Doumbia
Seydou, Gbohouo Guelassiognon Sylvain, Gosso Gosso Jean-Jacques, Kalou
Salomon Armand Magloire, N’dri Koffi Christian Romaric, Sangare Badra,
Serey Die Gnonzaroua Geoffroy, Sio Giovanni, Tiote Cheik Ismael, Toure
Yaya Gnegneri, Traore Lacina, Ya Konan Didier, Yao Kouassi Gervais na
Zokora Deguy Alain Didier.
Taifa
Stars iko kambini hoteli ya Tansoma tangu iliporejea kutoka Marrakesh,
Morocco ambapo leo na kesho itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 9 kamili alasiri. Ijumaa itapumzika, na itafanya
mazoezi ya mwisho Jumamosi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili.
Makocha
wa timu zote mbili (Taifa Stars na The Elephants) watakutana na
waandishi wa habari Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye
ukumbi wa mikutano wa TFF kuzungumzia jinsi walivyojiandaa kwa mechi
hiyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment