Habari kutoka Rwanda zinasema watu wasiopungua wanne wamepoteza maisha
baada ya jumba la ghorofa 4 kuporomoka katika mji wa Nyagatare,
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Habari zaidi zinasema zaidi ya watu
100 wamefukiwa kwenye vifusi. Wizara ya kukabiliana na majanga imesema
juhudi zinafanywa ili kuwaokoa wale waliofukiwa.
Jumba lililoporomoka
lilikuwa likiendelea kujengwa na baadhi ya watu wamedai kwamba vifaa
duni vilivyotumika huenda ndivyo vilivyosababisha jengo hilo kuanguka.
Msemaji wa Polisi, Theos Badege amethibitisha tukio hilo na kusema watu
21 wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya.
Badege amesema maafa
yanaweza kuwa makubwa kwani jengo hilo lilikuwa karibu na shule.
Shughuli za uokoaji zingali zinaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment