Moja ya Habari kubwa kwenye mitandao toka jana ni kuhusu mwigizaji wa
kike maarufu Angeline Jolie ambaye ni mke wa mwigizaji Brad Pitt kukatwa
matiti.Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja
na kuondoa mfuko wake wa uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New
York Times, Angeline Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na
kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani
ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angeline Jolie na familia yake ya watoto 6,ambapo 3 ni wakuzaa,3 ni wa 'kuadopt' na mume wake.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa
uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na
asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie.
Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.
"kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi"
Angeline Jolie na Mume wake Brad Pitt.
WITO:Kwa wanawake wote ni vyema mkafanye uchunguzi wa matiti yenu mapema
katika vituo vya afya ili kuoa maisha na kuzuia tatizo lisiwe
kubwa.Angeline Jolie ni mfano mzuri kwetu wanawake,ni ngumu lakini
inawezekana ukiwa na ujasiri mwisho wa siku unaokoa maisha yako.
0 comments:
Post a Comment