Mmoja kati ya watu kumi nchini Afrika kusini ana virusi vya HIV,
lakini vifo vinavyotokana na ukimwi vinapungua wakati matibabu
yanaanza kuonekana kuleta tija.
Afisa wa shirika la takwimu
nchini humo alisema jana kuwa baada ya miaka kadha ya
kuburuza miguu kuhusu mzozo wa HIV na ukimwi tangu mwaka
2004, Afrika kusini imetengeneza mpango mkubwa kabisa wa
matibabu ya HIV.
Ugonjwa huo utahusika na asilimia 32 ya vifo
mwaka huu. Licha ya kwamba kiwango hicho ni cha juu, lakini
ni upunguaji wa asilimia 48 kutoka viwango vya mwaka 2005.
Kiwango cha wastani cha maisha kimepanda hadi miaka 59.6
kutoka miaka 51.6 katika mwaka 2005.
Lakini kiwango cha
matatizo ni kikubwa, ambapo watu wapatao milioni 5.3 wanaishi
na na virusi vya HIV kutoka idadi ya wakaazi milioni 53 nchini
humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment