Tiketi
kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga
litakalochezwa keshokutwa (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza
kuuzwa kesho (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Vituo
vitakavyouza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni ni
Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni,
BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.
Tiketi
hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo
hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa
viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya
chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment