Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah
amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa
imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na
mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Amesema
awali Tanzania ilithibitisha kushiriki michuano kwa matarajio kwamba
Uganda ingekubali ombi la TFF la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN,
lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) likagoma kwa vile
kipindi ambacho kilipendekezwa lenyewe litakuwa na uchaguzi wa viongozi
wao.
Taifa
Stars itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi za CHAN ambapo mechi
ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu
wakati ya marudiano itafanyika jijini Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka
huu.
Akizungumzia
michuano ya COSAFA, Kocha Kim amesema angependa kushiriki michuano hiyo
kwani ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake, lakini kwa sasa malengo
makubwa ya Stars kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia na michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo fainali zake zitafanyika
mwaka 2015.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment