Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao chake na
wabunge wa CCM, katika ukumbi wa jengo la White House,
Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.
Wengine kushoto ni Spika wa Bunge
Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa
Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip
Mangula.
Wabunge
wa CCM wakiwa kwenye kikao chao na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya
Kikwete kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma.
Wajumbe
kwenye kikao cha Mwenyekiti wa CCM na Wabunge wakibadilishana mawazo ukumbini. Walioketi
mbele, Kushoto ni Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakiah Meghji na Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migoiro na Mbunge wa Urambo na
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC
Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata wakati wa kikao
hicho. Kushoto ni Mbunge wa Same Anne Kilango Malecela.
Mbunge
wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto)
akitaniana kuhusu Uyanga na Simba na Mwenyekiti wa Simba, Mbunge wa
Tabora Aden Rage nje ya ukumbi kabla ya kuanza mkutano huo. Kulia ni
Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya.
Picha kwa hisani ya vijimambo
0 comments:
Post a Comment