Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa
yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja
tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA
walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.
Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA
waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano
ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter
Kibatala na Naronyo Kicheere.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment