Muda umekwenda lakini
nimeona ni vyema tukashirikishana taarifa fupi tulizopata kutoka Afrika
Kusini anakotibiwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda kama nilivyoahidi.
1. Tangu
walipowasili jana katika hosipitali ya Milpark, Kibanda amekuwa
akiendelea na matibabu kwa maana ya kufanyiwa vipimo mbalimbali vikiwamo
CT Scan na X Ray hasa kichwani na sehemu nyingine za mwili ambazo
zilipata majeraha.
2.
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, jopo la madaktari wenye ujuzi wa
aina tofauti, walikuwa akitarajiwa kukutana ili kusoma taarifa ya
matokeo ya uchunguzi huo, ili kutafsiri maana ya matokeo hayo kisha
kutoa mwelekeo wa nini kinafuata au aina ya tiba anayopaswa kupata
Kibanda.
3.
Taarifa nyingine ni kwamba, imebainika kwamba mfupa laini (fizi)
uliopo kati ya pua na mdomo ni kama umekatika. Hii natokana na nguvu na
nyenzo walizotumia watesaji kumg’oa meno. Kutokana na hali hiyo ana
maumivu makali sana kwenye kinywa chake.
4. Pia
imebainika kwamba meno kama sita hivi katika kinywa cha Kibanda
yamelegea. Haya ni tofauti na yale mawili yaliyong’olewa katika tukio la
awali.
5. Kesho
Ijumaa Jukwaa la Wahariri litakutana katika mkutano wa wahariri wote
ili kujadili hatua zaidi za kuchukua kwa maana mbili; kwanza ni kuhusu
matibabu na afya ya Kibanda na pili usalama wa waandishi wa habari
kikazi.
6. Uongozi
wa Taasisi iitwayo Southern African Investigative Journalism Forum
umemtembelea Kibanda katika hosipitali ya Milpark na kueleza masikitiko
yake kuhusu yaliyomkuta. Wameahidi kushirikiana na taasisi za kihabari
za Tanzania, kuchunguza tukio hilo kwa lengo la kupata majawabu ya nini
kilichojiri na sababu za unyama huo.
Tutaendelea kuwaarifu hatua kwa hatua jinsi tutakavyokuwa tukipata taarifa kutoka Afrika Kusini.
--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment