Main Menu

Thursday, March 7, 2013

WANANCHI WA ZIMBABWE WAPIGWA MARUFUKU KUSIKILIZA RADIO ZA NJE YA NCHI

Serikali ya Zimbabwe ambayo inakaribia kuingia kwenye zoezi la kufanyika kura ya maoni na uchaguzi mkuu nchini humo, imeweka vizuizi kwa wananchi wake kusikiliza redio za kigeni. 

Polisi ya Zimbabwe imeeleza kuwa, ni marufuku kwa redio za nchi hiyo kusikiliza vituo vya kurushia matangazo vya kigeni, na hatua kali zitachukuliwa kwa mtu atakayekaidi agizo hilo. 

Duru za habari zinasema kuwa, serikali ya Zimbabwe haitaki wananchi wa nchi hiyo wasikilize sauti yoyote ya redio za kigeni isipokuwa redio ya taifa, ili wasisikie ukosoaji dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo. 

Hata hivyo Msemaji wa Polisi ya Zimbabwe amesema kuwa zoezi hilo limewekwa kwa minajili ya kuzuia vitendo vya uchochezi vinavyofanywa na vyombo vya kupasha habari vya kigeni dhidi ya serikali ya Zimbabwe.

radio tehran swahili

0 comments:

Post a Comment