Main Menu

Tuesday, February 19, 2013

MANISPAA YA IRINGA YAONGEZA MUDA WA KUFANYABIASHARA SOKO KUU MKOANI HUMO


                                                       mstahiki meya aman mwamwindi

             
Kukua na kuongezeko kwa idadi ya wakazi katika mji wa Iringa kumepelekea baraza la madiwani la manispaa hiyo kukubali ombi la wafanyabiashara wa soko kuu la kuongeza muda wa kufanya biashara.
 
Ombi hilo limepitishwa na kamati ya fedha na uongozi kwa niaba ya baraza la madiwani katika kikao chake kilichofanyika jana ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwezi.
 
Akizungumza na wanahabari mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi amesema, Manispaa imedhiria ombi hilo ambapo katika kuboresha mazingira ya soko hilo itaongeza taa na ulinzi kwa ujumla wakati wafanyabiashara wao watakua na jukumu la kulinda mizigo yao.
 
Aidha Mwamwindi amesema manispaa haijatoa kiasi chochote cha fedha katika mradi wa uwekaji taa kwenye baadhi ya barabara za manispaa hiyo bali ni makubaliano kati yake na muwekezaji, ambapo mwekezaji ameingia mkataba na makampuni ya biashara, makubaliano ya miaka mitatu.




  
     mstahiki meya manispaa ya iringa aman mwamwindi akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake


0 comments:

Post a Comment