Monday, January 14, 2013
WAASI WA SELEKA WA AFRIKA YA KATI WAMTEUA WAZIRI MKUU
Waasi wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamemteua Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni na serikali ya Rais Francois Bozize.
Nicolas Tiangaye mwanasheria wa mrengo wa upinzani aliyekuwa na nafasi muhimu katika mazungumzo ya amani ya waasi na serikali yaliyofanyika huko Libreville mji mkuu wa Gabon, amependekezwa na waasi hao kuchukua wadhifa wa Waziri Mkuu na sasa anasubiri tu kutangazwa rasmi na Rais Francois Bozize wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa makubaliano ya Gabon, Rais Bozize ataendelea kubakia madarakani hadi atakapomaliza muda wake mwaka 2016 lakini hatoruhusiwa kugombea Urais katika uchaguzi ujao.
Aidha Rais Bozize anapaswa kuvunja serikali ya sasa ili kuruhusu kuundwa serikali ya mpito ambayo itakuwa ni ya umoja wa kitaifa. Kadhalika mkataba huo unataka Waziri Mkuu achaguliwe kutoka mrengo wa upinzani ambaye ataongoza serikali ya mpito hadi uchaguzi wa Bunge utakapofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Na Radio Tehran
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment