Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, makumi kwa maelfu ya raia wa kaskazini
mwa Mali wameendelea kuyakimbia makazi yao wakihofia usalama wa maisha
yao kutokana na operesheni ya kijeshi dhidi ya makundi ya waasi katika
maeneo hayo.
Eduardo Del Buey, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaambia
wana habari kwamba, inakadiriwa kwamba, raia elfu thelathini
wameshayakimbia makazi yao kaskazini mwa Mali.
Msemaji wa Umoja wa
Mataifa amebainisha kwamba, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania
imethibitisha kuingia nchini humo maelfu ya wakimbizi wakitokea Mali.
Vikosi vya Ufaransa ambavyo viko nchini Mali kwa ajili ya kuvisaidia
vikosi vya serikali ya Bamako katika kupambana na makundi ya waasi ya
kaskazini mwa nchi hiyo, jana vilifanya mashambulio makubwa ya anga
katika ngome za waasi hao.
Wakati huo huo imeelezwa kwamba, baadhi ya
waasi wa kaskazini mwa Mali wamerejea nyuma kutoka katika maeneo
wanayoyadhibiti kufuatia kushadidi mashambulio ya anga ya majeshi ya
Ufaransa.
Waasi hao wamesema kwamba, hatua hiyo ni mbinu ya kivita na
sio kwamba, wamekimbia katika ngome zao.
CHANZO RADIO TEHRAN
0 comments:
Post a Comment