Rais Francois Hollande wa Ufaransa amekiri kuwa makomando wa
nchi yake wamepata pigo wakati wakijaribu kumkomboa jasusi Mfaransa
anayeshikiliwa mateka na wanamgambo nchini Somalia.
Katika taarifa Jumamosi jioni, Hollande amesema makomando wawili wa
kikosi maalumu cha Ufaransa waliuawa wakijaribu kumkomboa mateka ambaye
pia aliuawa katika oparesheni hiyo.
Wakati huo huo wanamgambo wa Al Shabab wanasema kuwa bado
wanamshikilia mateka huyo Mfaransa Denis Allex. Aidha wanamgambo hao
wamedai kuwa wamemchukua mateka mwanajeshi wa Ufaransa.
Oparesheni hiyo iliyofeli ya Jeshi la Ufaransa ilitekelezwa Jumamosi
alfajiri katika eneo la Buula-Marere yapata kilomita 110 kusini mwa mji
mkuu wa Somalia Mogadishu.
Walioshuhudia wanasema raia watano waliuawa
katika mapigano makali kati ya makomando wa Ufaransa na wapiganaji wa
Al-Shabab.
Allex alitekwa nyara na wapiganaji wa Al-Shabab Julai 2009
akiwa katika shughuli za ujasusi nchini Somalia.
CHANZO RADIO TEHRAN
0 comments:
Post a Comment