Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoondoka leo
jioni kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa
na mchezo dhidi ya Misri
Mart Nooij amesema watatumia kambi ya
Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, vijana wapo katika hali nzuri na
wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa
kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria, ikiwa ni
mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka
2017.
Kikosi cha Stars kinaondoka saa 11 jioni
kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa kuwasili jiji la Addis
Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini
Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji,
Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda,
Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon
Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma
Liuzio.
Msafara wa Taifa Stars
utaongozwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick
Nyange “Kaburu”.
0 comments:
Post a Comment