Main Menu

Friday, June 5, 2015

KIPA WA ARSENAL SZCZESNY MATATANI TENA KWA KUVUTA SIGARA HADHARANI



Pamoja na kukatazwa kuhusu uvutaji sigara, kipa wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny ameonekana tena akivuta sigara mbele za watu.

Kitendo hiki kinaweza kumuweka matatani kipa huyo mbele ya macho ya bosi wake Arsene Wenger.

Szczesny alishawahi kukonywa kuhusu uvutaji wa sigara na kutozwa faini ya pauni elfu 20 ikiwa ni siku moja baada ya Arsenal kufungwa na Southampton magoli mawili kwa sifuri.

Golikipa huyo hakuishia kutozwa faini tu bali pia alitemwa 
katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na kumpisha kipa mwezake David Ospina.
 
Safari hii Szczesny ameonekana akivuta sigara  mbele za watu akiwa na timu ya taifa ya Poland inayojiandaa na mchezo wa kufuzu kwa michuano ya Ulaya ya mwaka 2016.

Klabu ya Arsenal ipo katika mbio za kumpata kipa wa Chelsea Petr Cech ambaye mkataba wake unamalizika mwezi wa saba mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment