Morata ameifungia bao Juventus katika sare ya 1-1 katika Uwanja wa Bernabeu katika Nusu Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa.
Juve sasa inasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya magoli 3-2, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-1 mjini Turin.
Morata alitua kwa Kibibi Kizee cha Turin Julai 19 mwaka jana kwa dau la Euro Milioni 20 kwa Mkataba wa miaka mitano, huku Real Madrid ikipewa fursa ya kumnunua tena katika vipengele vya Mkataba.
Mechi ya kwanza alifunga pia dakika ya nane na mabao yake mawili yanakuwa mchango mkubwa kwa Juve kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambako watakutana na Barcelona iliyoitoa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3.
Fainali ya mwaka huu ya Ligi ya Mabingwa itafanyika Uwanja wa Olympia mjini Berlin, Ujerumani Juni 6, 2015.




0 comments:
Post a Comment