Pamoja na ushindi walioupata nyumbani usiku wa jana katika
Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya pili, timu ya Bayern Munich
imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matokeo
ya jana yanaifanya Bayern itupwe nje kwa kipigo cha jumla ya mabao 5-3, baada
ya awali kufungwa 3-0 Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.
Barca
sasa inamsubiri mshindi kati ya Real Madrid na Juventus katika mchezo
utakaopigwa leo.
Katika mchezo wa awali Juve ilishinda 2-1 nchini italia.
Mabao ya Bayern
katika mchezo wa jana yamefungwa na Medhi Benatia dakika ya saba,Robert
Lewandowski dakika ya 59 na Thomas Muller dakika ya 74, wakati ya Barca yote
yamefungwa na Neymar dakika ya 15 na 29.
0 comments:
Post a Comment