Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewaagiza wasimamizi wa vituo vya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kuhakikisha sheria na taratibu zote za mechi zinafuatwa.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu huu
2014/2015 inafikia tamati kesho (Mei 9, 2015) ambapo timu zote 14 zitakuwa
viwanjani katika mechi ambazo ndizo zitakazotoa hatma ya timu zinazoshuka
daraja.
Mechi hizo zitakuwa kati ya Ndanda na Yanga
(Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara), JKT Ruvu na Simba (Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam), Azam na Mgambo Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Stand United
na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Kagera Sugar na Tanzania
Prisons (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Mbeya City na Polisi Morogoro (Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa
Manungu, Morogoro).
0 comments:
Post a Comment