Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF, Mwesigwa Selestine ameomba radhi kwa vyombo kufuatia madai ya
waandishi wa habari kupata usumbufu wakati wa utoaji wa Zawadi kwa Mabingwa na
washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Mwesigwa alisema kwa niaba ya TFF anaomba
radhi kwa usumbufu wowote uliowapata waandishi na wadau wote walioshindwa
kushuhudia vema tukio hilo.
“TFF na FIFA vinatambua umuhimu na nafasi
ya wanahabri na vyombo vya habari si tu katika kuutangaza mchezo, bali pia
katika kutia chachu maendeleo ya mchezo wenyewe “ alisema Mwesigwa.
Hali mbaya ya hewa ilivuruga utaratibu
uliokuwa umepangwa awali kuanzia itifaki ya shughuli za kabla na wakati wa
mchezo na zile za utoaji tuzo.
Aidha Mwesigwa alisema TFF itaendelea
kushirikiana vema na jumuiya ya wanahabari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
kwamba wana mazingira mazuri wanapofanya kazi kwenye matukio ya mpira wa miguu.
0 comments:
Post a Comment