Kwa zaidi ya
asilimia 90 unaweza ukasema yanga ndio mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa
mwaka 2014/2015.
Hii inatokana
na matokeo waliyoyapata hii leo dhidi ya timu ya Ruvu Shooting kutoka mkoani
pwani katika muendelezo wa ligi kuu, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa.
Katika mchezo
huo yanga imeibuka na ushindi wa mabao 5 kwa bila na hivyo kuhitaji alama 3 tu
kuwavua ubingwa watetezi wa taji Azam Fc.
Yanga sasa
imefikisha alama 52 zikiwa ni 10 mbele ya Azam Fc japo Yanga ina mchezo mmoja
mkononi.
Magoli ya Yanga
hii leo yamefungwa na Simon Msuva na Kpah Sherman waliofunga magoli mawili kila
mmoja pamoja na goli la Amisi Tambwe.
Kwa magoli
hayo Msuva amefikisha magoli 16 na kujikita kileleni mwa wafungaji huku Tambwe akifikisha
magoli 11 katika nafasi ya pili.
Ligi hiyo
itaendelea kesho ambapo Azam Fc itawaalika Stand United, Simba Sc itakua
mwenyeji wa Ndanda fc, na Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar.
0 comments:
Post a Comment