Wakati viongozi wa
klabu ya soka ya Simba wakilalamika kushuka kwa mapato, Timu hiyo imetakiwa
kuwalipa wachezaji iliyovunja nao mkataba na kuwatoa kwa mkopo.
Agizo hilo
limetolewa na Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF likimhusisha mchezaji haruni chanongo .
Klabu hiyo inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni
Chanongo sh. 11,400,000, kufikia Aprili 30, 2015 ambayo ni leo vinginevyo
Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji
huyo.
Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao
kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba
kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi.
Kamati hiyo imeiagiza klabu ya Simba na klabu
nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho)
yote yalipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili
malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia
malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali ambayo inaweza msabababishia
usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.
0 comments:
Post a Comment