Hivi
inawezekana mashabiki wa Man U pamoja na benchi la ufundi linamkumbuka danny
welbeck katika kikosi chao baada ya kuwaadhibu usiku wa kuamkia leo?
Yawezekana likawa
ni swali unalojiuliza hivi sasa kutokana na mbadala wa Welbeck kushindwa
kutimiza lengo kusudiwa ndani ya kikosi cha Mashetani wekundu.
Wakati Danny
anaondoka Old Traford baadhi ya malegendary waliibuka na kuhoji kuuzwa kwa
mchezaji huyo aliyetafsiriwa kama nembo ya klabu kutokana na kukulia klabuni
hapo.
Kuondoka kwake
kulifungua milango kwa mshambuliaji raia wa Colombia Radamel Falcao aliyetua Traford
kuziba nafasi ya welbeck kitu ambacho kimeshindikana.
Falcao ameshindwa
kuonesha uwezo uliomridhisha Van Gaal ambaye amekua akimsugulisha benchi katika
michezo mingi ya mashindano mbalimbali na kuwapa nafasi washambuliaji Van Persie
na wayne Rooney.
Nimeanza na
swali kutokana na kile alichokifanya Welbeck jana usiku katika uwanja wake
aliouzoea akirudi kwa mara ya kwanza akiwa na timu tofauti na Man U.
Kwa matokeo
ya jana tunaweza kusema Arsenal itakua imetoka kwenye wingu la kipigo mfululizo
kutoka kwa Man U?
Danny Welbeck akifunga goli la ushindi la arsenal dhidi ya Manchester United usiku wa jana Old Trafford
David de Gea kipa wa man u akimtazama Welbeck akifunga baada ya kumpiga chenga
kocha wa United Louis van Gaal (kushoto) na msaidizi wake Ryan Giggs wakishuhudia kipigo
0 comments:
Post a Comment