Mshambuliaji
wa zamani wa vilabu vya Barcelona na Inter Milan Samuel Eto’o amepewa tuzo ya
ustamilivu yenye lengo la kupiga vita ubaguzi wa rangi na Shirika lisilo la
kiserikali linalofahamika kama Baraza la Maridhiano na Usuluhishi.
Sherehe za
tuzo hizo zilifanyika jana usiku katika ukumbi wa Kensington jijini London
nchini England, Eto’o aliambata na wachezaji wenzake Deco pamoja na Kolo Toure
ambao nao walikuwa sehemu ya wageni waalikwa.
Baada ya
tuzo hiyo,Eto’o alisema kuwa umefika wakati sasa adhabu za vitendo vya kibaguzi
kuwa kubwa ili kukomesha tabia hiyo.
Mwaka 2005
Eto’o akiwa na klabu ya Barcelona, alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki
wa Real Zaragoza ambao walikuwa wakifanya kejeli zinazofanana na nyani huku
zaidi wakimlenga Eto’o.
Tuzo zinazotolewa
na Baraza hilo zilianza rasmi mwaka 2010 na zilishuhudia Mfalme wa Hispania Juan
Carlos akichukua tuzo hiyo.
0 comments:
Post a Comment