Mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya ya Iringa Benitho Kayugwa akizungumza na uvccm baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku 5 kuhusu ujasiliamali, kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika katika kambi ya vijana ya Ihemi hivi karibuni.
baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya hiyo Benitho Kayugwa akimkabidhi cheti ya utambulisho wa mafunzo hayo Newton
(Picha zote na Denis Mlowe Iringa)
(Picha zote na Denis Mlowe Iringa)
========== ======= =========
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa wamemkataa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk. Leticia Warioba na kumuomba, Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa katika Wilaya hiyo na kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majuku yake na kutokuwa na ushirikiano kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Itikadi, Siasa,Utendaji na Ujasiliamali yaliyofanyika katika Chuo cha Vijana Ihemi kwa siku tano mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya hiyo Benitho Kayugwa, alisema Warioba hana ushirikiano katika kuwajibika na kutoa agizo ndani ya siku 60 serikali inayoongozwa na Jakaya Kikwete kuweza kumwondoa katika wilaya hiyo na kuwaletea mkuu wa wilaya anayejua wajibu wake katika kazi.
Kayugwa alisema wameamua kwa kauli moja kutokumtaka mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwa hana ushirikiano katika majukumu yake kulalamikiwa na wananchi pamoja na baadhi ya viongozi kwa kushindwa kuzingatia ushirikiano na kuendelea kukumbatiwa.
“Sisi Vijana wote tumeamua kwa pamoja tunataka kupata majibu ndani ya siku 60 kuweza kuondolewa kwa mkuu huyu wa wilaya ambaye anaonyesha kabisa kazi yake hawezi kuifanya na tutamgomea katibu yoyote atakayeletwa hapa wilayani hadi katibu aliyekuwa likizo ya miaka 3 apewe fedha zake kwenda kusoma, aidha kiongozi yoyote aliyechaguliwa na wananchi na hayuko tayari kuwajibika tuko tayari kumshughulikia ." alisema Kayugwa
Kayugwa aliitaka serikali kuwawajibisha watumishi wote wa vituo vya afya wanaokiuka maadili ya kazi kwa kuuza madawa ya serikali yanayotakiwa kupelekwa katika vituo vya afya na kushindwa kuyafikisha sehemu husika na kusababisha wananchi wasiwe na imani na serikali.
Aidha aliitaka serikali kuweza kuwajibisha viongozi wote wa ngazi tofauti ambao wanakiuka kuweka wazi matumizi na mapato ya kijiji kwa wananchi kwa kuwachukulia hatua kali kwa kuwa wanasababisha wananchi kuichukia serikali yao kutokana na uzembe wa watu wachache.
Aliongeza kwa kuiomba Serikali kuwahamisha watumishi waliokaa sehemu moja kwa muda mrefu kuwea kuleta mabadiliko chanya kutokana na baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mazoea na kufanya kazi pasipo weledi kwa kuzoea mazingira.
0 comments:
Post a Comment