Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi
wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini mwanza.
Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao
na kesi ikawa mahakamani na leo mchana mabina bila kibali cha mahakama
alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi wakaenda
kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo
ilhali kesi ipo mahakamani.? Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha
risasi hewani.
Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia m1 kwa risasi ndipo
wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na
kila dhana ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji
yametokea mchana huu majira ya saa 7.
Kamanda wa
polisi Mwanza amethibitisha japo hajasema nini chanzo cha mauaji.
chanzo jamiiforum
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment