Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi cheti kwa Meneja Rasilimali Watu Uhusiano wa Kibiashara (HR Business Partner) wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Emmanuel Christopher (kulia), baada ya kampuni hiyo kupata tuzo ya utoaji mafunzo na maendeleo kwa wafanyakazi yakiwemo ya elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Almas Maige, Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia Kabaka na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. Hafla hiyo ya kukabidhi tuzo kwa waajiri bora ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia akiipongeza TBL kupitia kwa Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo,Emmanuel Christopher
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. akiipongeza TBL kupitia kwa Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo,Emmanuel Christopher
0 comments:
Post a Comment