KUMEKUCHA ndani ya Mkoa wa Iringa, pale wanamitindo na wabunifu walio katika vyuo vikuu watakapochuana kesho katika tamasha la ‘Redd’s Uni-Fashion Bash’, ndani ya Ukumbi wa Shooter’s uliopo mjini hapa.
Tamasha hilo linalochochea vipaji ndani ya vyuo hivyo, awali lilifungua pazia ndani ya Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuhamia Kilimanjaro na litahusisha pia vyuo vilivyopo katika ndani ya Dar es Salaam.
Akizungumzia tamasha hilo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah alisema, wanafunzi wa vyuo vilivyopo mkoani humo ndiyo wakaoshiriki.
Wanafunzi wabunifu na wanamitindo wanaotarajiwa kushiriki tamasha hilo wanatoka Chuo Kikuu cha Iringa, Ruaha na Mkwawa huku burudani ikitolewa na msanii Joh Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’.
Fimbo alisema, wanafunzi wa vyuo vyote vya elimu ya juu walio na mapenzi katika ubunifu na mitindo wanatarajiwa kushiriki shindano hilo, huku akiamini kutakuwa na upinzani mkali zaidi ya ule wa Mwanza na Kilimanjaro.
Sh 500,000 wa pili Sh 400,000 mshindi wa tatu ataondoka na Sh 300,000 huku wanne na watano kila mmoja akipata Sh 100,000.
Kwa upande wa wabunifu mshindi wa kwanza atapata Sh 700,000 wa pili Sh 500,000 watatu Sh 300,000 na watakaokamata nafasi ya nne na tano watapata Sh 100,000 kila mmoja.
Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi alisema katika tamasha la leo, ana uhakika mkubwa wa kuwepo na upinzani wa kutosha mno.
“Tunataka kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo, kwa sasa wanafunzi katika mikoa iliyobaki wanatakiwa wajiandae mno, maana kuna upinzani mkubwa,” alisema Edith.
Kinywaji cha Redd’s Original pia ndicho kinachodhamini shindano la Redd’s Miss Tanzania na kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 comments:
Post a Comment