BAO
pekee la Aaron Ramsey dakika ya 62, limeipa Arsenal ushindi wa 1-0
ugenini dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund nchini Ujerumani.
Hilo
linakuwa bao la 13 kwa mchezaji huyo msimu huu na bao la tano katika
michuano ya Ulaya msimu huu. Pamoja na kufungwa, wenyeji ndio waliocheza
vyema usiku huo kabla ya Arsenal kupata bao lake, hawakuweza
kutengeneza nafasi hata moja ya kufunga.
Borussia
ambayo inapewa sifa ya moja ya timu bora kabisa Ulaya kwa sasa,
iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 6-1 dhidi
ya Stuttgart katika ligi Bundesliga, lakini ilikalishwa na
mtutu mmoja wa bunduki.
Dortmund;
Weidenfeller 6, Grosskreutz 7, Papastathopoulos 6, Subotic 7, Schmelzer
6, Sahin 5, Bender 5 (Hofmann 75, 5), Blaszczykowski 6 (Aubameyang 74,
5), Mkhitaryan 6, Reus 6 (Schieber 86), Lewandowski 6.
Arsenal:
Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta,
Cazorla/Monreal dk75, Ozil, Rosicky/Vermaelen dk91 na Giroud/Bendtner
dk90.
Ramsey akifunga bao muhimu
Dortmund ilipata nafasi nyingi nzuri ikapoteza
MECHI ZILIZOBAKI ZA ARSENAL:
Marseille (H), Novemba 27
Napoli (A), Desemba 11
Napoli (A), Desemba 11
Katika
mechi nyingine, Barcelona imeifunga AC Milan mabao 3-1 Uwanja wa Camp
Nou, Lionel Messi akifunga mawili dakika ya 30 na 83, wakati lingine
limefungwa na Busquets dakika ya 40, huku Pique akijifunga dakika ya 45
kuwapatia wageni bao la kufutia machozi.
Barcelona:
Valdes; Dani Alves, Pique, Mascherano, Adriano; Xavi/Song dk88,
Busquets, Iniesta/Fabregas dk78, Alexis, Messi na Neymar/Pedro dk85)
AC
Milan: Abbiati; Abate, Zapata, Mexes, Emanuelson; Muntari, Montolivo,
De Jong, Poli/Birsa dk74', Kaka/Matri dk84, Robinho/Balotelli dk46.
Nyota wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akishangilia bao lake la mwisho na mpishi wake, Cesc Fabregas
Messi akifunga bao la pili
Nayo Chelsea imeifumua 3-0 Schalke 04, mabao ya Samuel Eto'o dakika ya 31 na 54 na Demba Ba dakika ya 83.
Chelsea:
Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Mikel, Cahill, Terry, Willian, Ramires,
Eto'o/Ba dk77, Oscar/Lampard dk81 na Schürrle/De Bruyne dk78.
Schalke:
Hildebrand, Uchida, Aogo, Neustädter, Höwedes, Matip, Draxler/Clemens
dk62, Jones, Szalai, Boateng/Kolasinac dk77 na Fuchs/Meyer dk67.
Samuel Eto'o aliuzuia mpira wa Timo Hildebrand kabla ya kuifungia Chelsea baola kwanza
Eto'o akishangilia na kocha Jose Mourinho
Eto'o akifunga la pili
Willian akimpongeza Eto'o
Demba Ba akifunga bao la tatu
Ba akishangilia bao lake
0 comments:
Post a Comment