Zaidi ya wakurugenzi 24 wa halmashauri nchini wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu huku wengine wakifukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha za miradi ya maendeleo ya miji.
Sambamba na hao zaidi ya wakuu 75 wa idara zilizo chini ya halmashauri hizo nao wamehusishwa na kadhia hiyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi
2012.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mkuu wa kitengo cha mawasiliano ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Rebecca Kwandu wakati akizungumzia miradi ya maendeleo ya miji nchini.
Ametaja baadhi ya changamoto zinazoikabili serikali katika maendeleo ya miji nchini ikiwa ni pamoja na ongezeko la watu kuhamia mijini, miundombinu isiyokidhi matumizi ya miji, uwezo mdogo wa kifedha na kuongeza kuwa mpaka kufikia 2030 zaidi ya watu milioni 25 watakuwa wanaishi mijini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment