Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu
uliofanyika siku chache zilizopita nchini humo na mahudhurio makubwa ya
wananchi kwenye zoezi hilo ni jibu kali kwa siasa za nchi za Magharibi.
Mugabe amesema kuwa matokeo ya uchaguzi huo na jinsi wananchi
walivyoshiriki kwa wingi katika zoezi hilo vimezivunja moyo nchi za
Magharibi.
Ameongeza kuwa nchi za Magharibi ni maadui wa Zimbabwe na
kwamba wananchi wametoa kipigo kikali kwa siasa za nchi hizo dhidi ya
Zimbabwe.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe,
Rais Robert Mugabe alimshinda mpinzani wake mkubwa Morgan Tsvangirai wa
chama cha MDC kwa kupata asilimia 61 ya kura.
Chaguzi za Rais na Bunge za Zimbabwe zilifanyika tarehe 31 mwezi uliopita wa Julai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment