Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Thomas Mihayo amesema kushamiri kwa matukio ya uuzwaji, ununuaji wa dawa za kulevya, sambamba na upitishaji wa dawa hizo katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini, kunachangiwa na rushwa iliyokithiri katika Mahakama na Polisi.
Amesema matukio mengi ya mauaji ya raia wasio na
hatia pamoja na upitishwaji wa wanyamapori (Twiga) katika viwanja vya
ndege mbalimbali nchini hayachukuliwi hatua stahiki kwasababu rushwa
imetawala, “Kuzungumzia rushwa siyo hoja, tatizo ni kuwa matendo yetu ni
tofauti na kauli tunazotoa.” Katika maelezo yake alisema anamuonea
huruma Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kwani licha ya
kuonyesha wazi kutaka kupambana na watu wanaoingiza dawa za kulevya
kupitia katika viwanja vya ndege, hataweza kwa maelezo kuwa rushwa ndiyo
inafanikisha mipango yote ya uingizwaji wa dawa hizo.
Jaji Mihayo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) aliyasema hayo jana katika
mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, huku akitoa mifano ya kesi
mbalimbali ambazo watuhumiwa waliachiwa huru katika mazingira
yanayoonekana wazi kuwa Mahakimu walipewa rushwa.
“Twiga kusafirishwa kupitia viwanja vya ndege
maana yake ni rushwa ilitembea na siyo uzembe.
Sasa tunaona mauaji ya watu wasio na hatia lakini vyombo vya dola vinafumba macho na hakuna kinachofanyika.Katika nchi inayofuata sheria mambo kama haya lazima yafanyiwe kazi, lakini ukiona kimya maana yake rushwa imetawala” alisema na kuongeza;
Sasa tunaona mauaji ya watu wasio na hatia lakini vyombo vya dola vinafumba macho na hakuna kinachofanyika.Katika nchi inayofuata sheria mambo kama haya lazima yafanyiwe kazi, lakini ukiona kimya maana yake rushwa imetawala” alisema na kuongeza;
“Rushwa imetoka huko sasa imeingia katika dawa za
kulevya, Watanzania wengi wanadhani dawa za kulevya kupita katika uwanja
wa ndege ni uzembe wa wasimamizi, hilo siyo kweli yamepita kwa sababu
ya rushwa.”
“Hawa watu polisi wanawajua lakini wanawalinda…, ndiyo wanalindwa na haohao polisi” alisisitiza.
Akitolea mfano tukio la Julai 5 mwaka huu la
upitishaji wa mabegi tisa ya dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) lililoanikwa na hadharani na
Dk Mwakyembe, ambapo watu mbalimbali walitajwa kuhusika, wakiwemo
maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao walidaiwa kuchelewesha mbwa
kwa ajili ya kukagua mizigo alisema, “Mbwa hawawezi kupokea rushwa na
kama wangekuwepo katika uwanja wa ndege. Ni wazi kuwa wangeweza kubaini
dawa hizo za kulevya.”
Alifafanua, “Dk Mwakyembe alieleza wazi kuwa mbwa
walichelewa kufika uwanja wa ndege, swali la kujiuliza kwa nini
walichelewa? Sababu za kuwachelewesha zinaweza kuwa nyingi tu, unaweza
kusema gari liliharibika.”
Alisema haoni uwezekano wa Dk Mwakyembe kufanikiwa
katika mapambano hayo, kwani hata kama viwanja vya ndege vitafungwa
mashine za kubaini waliobeba dawa hizo, kama wasimamiaji watapokea
rushwa hakuna atakayekamatwa.
“Kama kutakuwa na sheria kali za kudhibiti dawa za
kulevya basi watekelezaji wa sheria hizo wanatakiwa kuwa waaminifu na
kuichukia rushwa.
Pia tunaweza kuwa na sheria kali lakini ndiyo rushwa ikaongezeka zaidi” alisema Jaji Mihayo
Pia tunaweza kuwa na sheria kali lakini ndiyo rushwa ikaongezeka zaidi” alisema Jaji Mihayo
“Watanzania watafanikiwa kuikomesha rushwa kama
wakiichukia.
Nasema hivi kwa sababu siku hizi mtu aliyekithiri kwa kupokea rushwa anashabikiwa na wenzake. Mahakama zetu nazo zinatakiwa zitekeleze wajibu wake ipasavyo” alisema
Nasema hivi kwa sababu siku hizi mtu aliyekithiri kwa kupokea rushwa anashabikiwa na wenzake. Mahakama zetu nazo zinatakiwa zitekeleze wajibu wake ipasavyo” alisema
Rushwa katika Mahakama
Huku akitoa mifano halisi, Jaji Mihayo alisema
kuwa hivi karibuni alisomewa hukumu moja ya kesi ya dawa za kulevya na
Dk Mwakyembe, hukumu aliyodai kuwa inaonekana wazi hakimu alipewa
rushwa.
Bila kutaja Mahakama wala hakimu aliyetoa huku
hiyo alisema, “ Kuna mtu mmoja alikamatwa na dawa za kulevya akiwa
amezimeza baadaye alifikishwa mahakamani huku dawa zile alizokutwa nazo
zikitumika kama ushahidi,”
“Cha ajabu wakati wa hukumu ya kesi hiyo hakimu
alimuachia huru mtuhumiwa kwa maelezo kuwa hakukuwa na ushahidi wa
kutosha kwamba dawa zile za kulevya zilikuwa zimemezwa na mtuhumiwa
huyo. Mimi ni Jaji nilisikiliza uchakachuaji wa kesi hiyo nilijua tu
kuna rushwa ilitembea.”
Alisema kesi nyingine ambayo uamuzi wake ulikuwa
ya utata, alielezwa na ofisa mmoja wa Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana
na Rushwa (Takukuru).
“Yule ofisa wa Takukuru alinieleza kuwa kuna jamaa
mmoja aliombwa rushwa na Sh1milioni. Kutokana na hali hiyo mtu huyo
alikwenda kuripoti Takukuru ambao waliandaa mpango wa kumkamata mwomba
rushwa kwa kumweka mtego wa Sh500,000” alisema na kuongeza;
“Yule mtu aliyeomba rushwa alikamatwa na
kufikishwa mahakamani, ila cha kushangaza hakimu alimwachia huru
mtuhumiwa, kwa maelezo kuwa aliomba Sh1 milioni lakini alipewa
Sh500,000.
Hiki ni kichekesho kweli yaani kwasababu fedha aliyoomba siyo aliyopewa basi akaachiwa huru.”
NA gazeti mwananchi
Hiki ni kichekesho kweli yaani kwasababu fedha aliyoomba siyo aliyopewa basi akaachiwa huru.”
NA gazeti mwananchi
0 comments:
Post a Comment