Msanii
wa muziki wa kizazi kipya ambaye amezidi kujijengea heshima ndani na
nje ya nchi Nasib Abdul maarufu kama Diamond anatarajiwa kupagawisha
wakazi wa mkoa wa Kigoma Jumamosi hii na style ya kipekee ya ‘Kikwetu
Kwetu’ kwa hisani ya bia ya Kilimanjaro.
Msanii
Diamond ataungana na wasanii wengine tisa wa muziki wa Bongo Fleva
watakaotumbuiza katika tamasha la ‘Kili Music Tour 2013’ ambalo
linatarajiwa kufanyika mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika
siku ya Jumamosi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bwana
George Kavishe alisema kuwa “tamasha la Kili Music Tour linaelekea
Kigoma baada ya kufanya vizuri jijini Mbeya, Mwanza, Dodoma, Tanga na
Kilimanjaro. Wasanii kumi ambao watatumbuiza Jumamosi hii ni Diamond
Plutnumz, Linex, Barnaba, AT, Fid Q, Prof J, Recho, Lady Jay Dee, Roma
na Ben Paul.”
Bwana
Kavishe aliendelea kufafanua kuwa amefurahishwa sana na jinsi
watanzania wanavyopokea bonge la kiburudisho kutoka kwa bia yao ya
Kilimanjaro. “ni faraja kubwa kuona jinsi style ya “kikwetukwetu”
ilivyokubalika nchini kote. Kilimanjaro inaelewa fika kuwa watanzania
wana mambo mengi sana ya kujivunia ambayo ni ya kipekee kikwetukwetu.
Ukiachana
na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo inatengenezwa Tanzania, na
watanzania, kwa viungo vya kitanzania kwa ajili ya watanzania, kuna
mambo mengine mengi sana ya kikwetu kwetu kama muziki wetu wa bongo
fleva, dansi zetu za kiduku, kandanda letu na ushindani wa Simba na
Yanga, komedi yetu iliyo tofauti kabisa n.k. “
Kwa
upande wake Diamond alisema kuwa “Kama ilivyo kauli mbiu ya tamasha
hili ‘Kikwetu kwetu’ naamini nitatoa burudani kali kabisa kwa
wanakigoma. Ukizingatia kuwa Kigoma ni nyumbani wanandugu zangu
wategemee bonge la kiburudisho kutoka kwangu na wasanii wenzangu
nitakaokuwa nao”.
0 comments:
Post a Comment