Katika kile kinachoonekana ni kuendelea kuzorota uhusiano wa Nairobi
na Washington, maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Kenya wamesusia
sherehe za uhuru wa Marekani zilizofanyika jana usiku katika ubalozi wa
Marekani mjini Nairobi.
Katika hafla hiyo ambayo maafisa wote wa ngazi za juu serikalini
walialikwa, rais na naibu wake hawakuhudhuria, aidha hakuna waziri au
katibu mkuu wa wizara aliyehudhuria hafla hiyo.
Sherehe hizo zimekuja
siku mbili tu baada ya Rais Obama kukamilisha safari yake ya
kuzitembelea nchi za Afrika pasina kuitembelea Kenya kama
ilivyotarajiwa.
Afisa pekee wa serikali ya Jubilee aliyehudhuria sherehe
hizo ni Spika wa Senate Ekwe Ethuro na maafisa wa ngazi za chini kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje.
Hivi karibuni Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake
haibabaishwi na mitazamo ya nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikimpiga
vita.
Rais Kenyatta alisema mitazamo ya nchi za Magharibi haitaizuia
serikali ya Jubilee kuwahudumia Wakenya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment