Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah akikabidhi kombe la ubingwa kwa timu ya Mbaspo kutoka Mbeya baada ya kufanikiwa kushindwa kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya wahasimu wao Mbeya City katika faili ya kombe la Muungano Mufindi 2013 na kunyakua kombe na pesa kiasi cha Tsh milioni 3
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mbeya kushoto akiwa na mmoja kati ya wachezaji wa timu ya Mbaspo wakionyesha kombe la ubingwa leo katika uwanja wa shule ya Msingi Wambi mjini Mafinga.
Mabingwa wa mashindano ya kombe la Muungano Mufindi mwaka 2013 timu ya Mbaspo ya Mbeya katika picha ya pamoja na mashabiki wageni rasmi na wadhamini jioni ya leo katika uwanja wa Wambi mjini Mafinga.
Timu ya Mbaspo kutoka mkoani Mbeya jana imeibuka bingwa wa mashindano ya kombe la Muungano 2013 baada ya kuigagadua kwa jumla ya mikwaju ya panelt 5-4 timu ya Mbeya City katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Shule ya Msingi Wambi mjini Mafinga mchezo ulioshuhudiwa na mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza timu ya Mbaspo imekabidhiwa pesa kiasi cha Tsh milioni 3 Mendani na kombe ,mshindi wa pili Mbeya City akinyakua mendani na Tsh milioni 1.5 wakati mwamuzi bora na mchezaji bora kila mmoja akinyakua Tsh 400,000
Mratibu wa mashindano hayo Daud Yassin Amewapongeza wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo kampuni ASAS LTd ya Iringa,kampuni ya Mwananchi Communication,NSSF,Pareto, Ibrahim Khamis, PPF,MUcoba Benk na Chai Bora kwa kufanikisha mashindano hayo.
Na Francis GodwinBlog
0 comments:
Post a Comment