Ikiwa zimebaki wiki
mbili tu Shawn Corey Carter a.k. Jay-Z aingize sokoni album yake ‘Magna Carta
Holy Grail’ameamua kuweka wazi majina ya ngoma zote 13 zitakazokuwa kwenye
album hiyo.
Jigga amewapa fans wake maelezo ya ziada kuhusu kila wimbo,
na inaonekana mashabiki wake wana usongo wa kujua ni mashairi ya aina gani
yatasikika kwenye album hiyo na kama inavyoeleweka Jamaa huwa hakosei kufanya
hit karibia album nzima.
Magna Carta Holy Grail itaingia mtaani July 4 ambapo wateja
wa simu aina ya Sumsang watakuwa wa kwanza kuipata album hiyo tena bure kwa
kudownload tu applications za simu hiyo, na kisha fans wengine wataanza kuipata
kuanzia July 7.
Kumbuka Magna Carta ilikuwa ni document ya kwanza mwaka
1215, iliyomlazimisha mfalme wa Uingereza kutumia utawala wa sheria na hivyo
kumpunguzia mamlaka binafsi, na hiyo ilisaidia sana kuleta hiki ambach
tunajivunia sasa ‘Utawala wa sheria’. Anyways tuachane na historia.
Hii ndiyo list ya ngoma 13 zitakazoijaza ‘Magna Carta Holy
Grail’:
1. Picasso Baby
2. Heaven
3. Versus
4. Tom Ford
5. Beach Is Better
6. F--kWithMeYouKnowIGotIt
7. Oceans
8. F.U.T.W.
9. Part II (On The Run)
10. BBC
11. La Familia
12. Jay-Z Blue
13. Nickles & Dimes
pia Jay Z ametoa lyrics za wimbo unaoitwa “Holy Grail” aliyomshirikisha Justin Timberlake utakaokuwemo katika album hiyo. Wimbo huu ameu sample kutoka katika wimbo wa Nirvana “Smells Like Teen Spirit”.
Sio mbaya ukijitengenezea beat yako kichwani na melody wakati unayasoma mashahiri haya kabla hujausikia wimbo kamili (July 7) album ya ‘Magna Carta Holy Grail’ itakapotoka rasmi.
0 comments:
Post a Comment